• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MCHINA kuanza kuweka lami nzito Songea

Tarehe ya kuwekwa: March 22nd, 2018

HATIMAYE Kampuni ya kimataifa ya China inayoitwa China Sichuan International Co-operation Machi 25 mwaka huu inaanza rasmi  ukarabati wa barabara za Manispaa ya Songea kwa kiwango cha lami nzito.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya  amesema Kampuni hiyo tayari imesaini mkataba baina ya Kampuni hiyo na Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo mkataba unaonesha kuwa ukarabati wa barabara hizo zenye urefu wa kilometa 10.3 unaanza Machi 25,2018 na unatarajia kukamilika  Septemba 30,2019.

“Mkataba ni wa miezi 18,fedha ambazo zinatumika katika ukarabati huo ni bilioni 10.96,Mkandarasi wa sasa anaongeza kilometa zaidi ya mbili,pia ataweka taa za barabarani’’,amesema Mhandisi Sanya.

Halmashauri ya Manispaa ya Songea  ilivunja  Mkataba wa ujenzi wa lami nzito yenye urefu wa kilometa 8.6 kati yake na Kampuni ya Lukolo yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam,baada ya Kampuni hiyo kukiuka masharti ya mkataba wa miaka miwili  uliomalizika Juni 30 mwaka 2017.

Baada ya muda huo kumalizika Mkandarasi huyo aliingizwa kwenye tozo(Liquidated Damage) kwa siku 100 ambapo Oktoba 8,2017 ndiyo siku 100 alizopewa Mkandarasi huyo zilimalizika hivyoManispaa ilivunja mkataba rasmi na Kampuni ya Lukolo.

Baada ya kuvunjwa mkataba huo,Manispaa ya Songea ilianza mchakato wa kumtafuta Mkandarasi mwingine ambapo amepatikana Mkandarasi wa Kampuni ya China Sichuan International ambaye ataendeleza kazi ya ukarabati barabara na kwamba Manispaa haijapata hasara yeyote baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa Mkandarasi wa kwanza.

Fedha za mradi huo ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 14 zimetolewa na Benki ya Dunia chini ya Mpango wa kuzijengea uwezo serikali za mitaa(ULGSP), mpango huo unakusudia kuendeleza miundombinu ya Halmashauri za miji na Manispaa 18 za Tanzania Bara ikiwemo Manispaa ya Songea.

Mradi huo ambao ulianza Juni Mosi 2015 ulitarajiwa kukamilika Juni 30,2017.Barabara za Manispaa ya Songea ambazo zipo kwenye mradi huu ni FFU hadi Matogoro yenye urefu wa kilometa 3.2,barabara ya Songea Girl’s hadi Mateka yenye urefu wa kilometa 1.5 na barabara ya Mwembechai hadi Bombambili yenye urefu wa kilometa 2.6.

Barabara nyingine ni Mitumbani hadi Yapenda yenye urefu wa kilometa moja,barabara ya Polisi hadi Stendi ya Mlilayoyo yenye urefu wa kilometa 0.45.

Taarifa imetolewa na Albano Midelo

Afisa Habari Manispaa ya Songea

Machi 22,2018                                           

 

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa