Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassan Mshaweji amewaasa watalaam kuondoka katika mfumo wa uendeshaji wa vikundi wa zamani na kuingia katika mfumo mpya ambao unazingatia sayansi, teknolojia, utawandawazi na soko huru.
Anasema mfumo mpya wa mikopo kwa wajasirimali wadogo utakuwa na manufaa kwa walengwa na wateja wao hasa katika soko huru ambalo linaushindani mkubwa na kwamba njia pekee ya kupambana na soko huru ni Sayansi na teknolojia.
“Ili kuhakikisha biashara zenu zinafanyika vizuri ni lazima mzingatia ubora wa bidhaa mnazozalisha,bei,eneo la biashara,aina ya wateja wako na kuitangaza biashara yako ili wateja waweze kufahamu na kununua’’,anasema Mshaweji.
Mstahiki Meya pia amewakumbusha wajasirimali wadogo kuwa na tabia ya kuweka akiba mara kwa mara,kukopa kwa busara na kulipa na kufanya marejesho ya mikopo kwa wakati ili iweze kukopeshwa kwa vikundi vingine.
Anasisitiza kuwa bila marejesho kwa wakati,Halmashauri haitakuwa na uwezo wa kutoa mikopo mingine kwa vikundi vingine hivyo anatoa rai kwa vikundi hivyo kubadilika kwa kurejesha mikopo ili iwanufaishe wengine.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya anasisitiza kuwa kila mwak Manispaa itaendelea kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo katika vikundi vya wajasirimali wadogo vya vijana na wanawake.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa