Neil Amstrong wa nchini Marekani alifariki dunia mwaka 2012 baada ya kutokea matatizo akifanyiwa operasheni ya moyo.Neil Amstrong ni binadamu wa kwanza kufika mwezini, alifariki akiwa na miaka 82.Dunia itamkumbika kwa rekodi yake ya kihistoria ya kuwa binadamu wa kwanza kuingia na kukanyaga mwezini.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji BBC,Safari hiyo ya kutumia chombo cha masafa marefu kinachoitwa Apollo 11 ilifanyika mwaka 1969 ,Amstron akiwa kiongozi wa msafara wa watu watatu kuelekea mwezini.
Ilikuwa Julai 6 1969 waliondoka huku wakipunga kuaga na Amstrong akiwa mbele kabisa kuingia kwenye van iliyowapeleka kwenye rocket tayari kuanza safari kuelekea mwezini. Neil Amstrong na mwenzake Buzz Aldrin wakiwa mwezini waliweka bendera ya Marekani.Walikaa mwezini kwa saa tatu tu.
Neil Amstrong alikanyaga kwa mara ya kwanza mwezini yeye akiwa wa kwanza Julai 20 1969,Buzz Aldrin yeye alikuwa wa pili kukanyaga mwezini nyuma ya Neil japo wote walikuwa katika mission moja hiyo ya Apollo 11.
Kulingana na wasifu wa Armstrong ambao umechapishwa na shirika la anga la Marekani, NASA, mwanaanga huyo aliyezaliwa jimboni Ohio mwaka 1930, alisafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza akiwa na miaka sita, na kupata leseni ya kuendesha ndege akiwa na miaka 16, hata kabla ya kujua kuendesha gari.
Alitumikia jeshi la Marekani kama rubani wa ndege za kivita wakati wa vita vya Korea, na baadaye akajiunga na masomo ya sayansi ya anga. Baadaye aliajiriwa kama rubani wa kuzifanyia ndege majaribio. Neil Armstrong alijiunga na programu ya anga mwaka 1962, na kurusha chombo cha kwanza cha anga miaka minne baadaye.
Aliteuliwa kuwa kiongozi wa wanaanga walioshiriki katika safari ya Apollo, ambayo iliwafikisha wanadamu wa kwanza mwezini. Hatua yake ya kwanza mwezini iliangaliwa na mamilioni ya watu duniani kwa njia ya televisheni.
Imeandaliwa kwa msaada wa mitandao na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Mei 13,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa