Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa ya Juni 2018 ambapo imeelezwa kuwa mfuko wa bei umepungua hadi kufikia asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 3.6 ilivyokuwa Mei 2018.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Juni 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2018.
NBS imebainisha kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula ambazo ni bia kwa asilimia 1.1, gharama za ukarabati wa vifaa vya umeme na viyoyozi kwa asilimia 1.8, gesi za kupikia majumbani kwa asilimia 5.6, majiko ya mkaa kwa asilimia 2.0 na gharama za mawasiliano kwa asilimia 2.6.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 11,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa