MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Songea mjini Tina Sekambo (pichani) amemtangaza Dk.Damas Ndumbaro wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Songea mjini baada ya kupata jumla ya kura 45,762 sawa na asilimia 96.4 ya kura halali zilizopigwa na jumla ya wapiga kura 47,600.
Sekambo amesema katika jimbo hilo jumla ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 128,841 ambapo jumla ya vyama kumi vilijitokeza kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Kwa mujibu wa Sekambo matokeo ya wagombea wa vyama vingine ni Christina Chinangwa wa CUF amepata kura 608,Neema Tawete wa ADA-TADEA amepata kura 471 na Mgombea wa AFP Abdul Ngakolwa amepata kura 374.
Sekambo amemtaja Mgombea wa CCK Mayono Rashid amepata kura 59,Mgombea wa DP Steven Ndumba amepata kura 56,Mgombea wa Chama MAKINI Abdalah Ngonyani amepata kura 22,Mgombea wa NRA Hamis Kassian amepata kura 20,Mgombea wa TLP Photina Kapinga amepata kura 53 na Mgombea wa Chama cha UPDP Juma Mbawala amepata jumla ya kura 30.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa