Naibu Meya manispaa ya Songea Jeremia Mirembe ambaye pia ni Diwani wa kata ya Bombambili ameungana na wananchi wa kata ya Bombambili katika kufanya maombolezo ya kifo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifariki tarehe 17.03.2021 na kuzikwa 26/03/2021 Chato Mkoani Geita.
Jeremia amefanya maombolezo hayo leo 26.03,2021 katika ukumbi wa ofisi ya kata Bombambili yaliyohudhuriwa na wananchi mbalimbali, viongozi wa vyama vya siasa kata/ wilaya na vongozi wa dini kwa lengo la kuunga mkono maombolezo ya kifo cha Rais Dkt. John pombe Magufuli.
Jeremia alisema Kifo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni pigo kubwa kwa Taifa letu kutokana na mambo mengi mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake ikiwemo na kutuunganisha kuwa kitu kimoja.
Alisema amefunga luninga hiyo ukumbini hapo kwa lengo la kuwasaidia wananchi wenye mapenzi mema ambao wanahitaji kuangalia luniga ili waweze kushiriki mazishi kama chato.
Amewata wananchi hao kuendelea kufanya maombolezo kwa kupitia jumuyia za dini mbalimabli au nyumba za ibada ili kumuombea kiongozi wetu jemedali, na mtetezi wa wananchi wanyonge.
Naye mwenyekiti wa CCM kata Bombambili Omary Nchimbi amewataka wananchi kulinda na kutunza yale yote yaliyofanywa na kiongozi huyo na pia na iwe mfano wa kuigwa.
Naye mwenyekiti wa UVCCM Songea mjini Kelvini K. Chale alisema hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa kiongozi mpenda haki, muwazi, mchapakazi, mtetezi wa wanyonge na alichukia ufisadi.
Nao wananchi wa kata ya Bombambili wakizungumza kwa wakati tofauti ambapo walisema hayati Dkt. John Pombe Magufuli atakumbukwa kwa mambo mengi mazuri kama kupokea kero na kuzitolea ufumbuzi hapohapo, ujenzi wa barabara iendayo bombambili - mwembechai ambayo imekamilika na inatumika.
iMEANDALIWA
AMINA PILLY.
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
26.03.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa