Kauli hiyo imetamkwa hapo jana 15.09.2020 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika tarehe 28 octoba mwaka huu uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe Manispaa ya Songea.
Mh. Samia alianza kwa kutoa shukrani kwa wananchi wa Manispaa ya Songea kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi wenye lengo kuu la kuwaeleza wananchi mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano chini ya uongozi wa Dr. John Pombe Magufuli.
Alisema katika sekta ya kilimo Serikali imejipanga kuagiza pembejeo za kilimo ili wakulima wapate pembejeo kwa wakati na kwa sifa zinazotakiwa na kwa bei nafuu.
Alisema kwa miaka mitano iliyopita waliweza kushusha bei ya mbolea kutoka shilingi 64,000/= hadi shilingi 46,000/=. Pia Serikali imejipanga kuwezesha uwekezaji wa kilimo cha biashara kwa kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao gharani na kujenga na kukarabati maghala yenye tani 531850 pamoja na kuweka mfumo mzuri wa soko la ndani na soko la nje.
Aidha katika sekta ya elimu Mkoa wa Ruvuma umepokea zaidi ya bilioni 26 kwa ajili ya ujenzi, ukamilishaji, na ukarabati kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Alisema jumla ya shilingi bili 42 zilitolewa kwa ajili ya elimu bure bila maliopo. Aliongeza kuwa Serikali isingetoa fedha hizi, fedha hizo zingetolewa na wazazi wa wanafunzi, hivyo Serikali ikaona ni vyema sasa fedha hizo zitolewe na Serikali ili kuwapunguzia mzigo huo wazazi kwa ajili ya elimu ya watoto wetu kwa elimu msingi na sekondari.
Hata hivyo, alifafanua kuwa Mkoa wa Ruvuma mwaka 2015 ulikuwa na shule za Msingi 670 hadi kufikia 2020 shule zimeongezeka na kufikia shule 800, pia kwa upande wa shule za sekondari mwaka 2015 kulikuwa na shule 111 hadi kufikia mwaka 2020 shule zimeongezeka na kufikia idadi ya shule 205.
Aliongeza kuwa zaidi ya billion 9 zimetumika kujenga madarasa 433, nyumba za walimu 46, matundu ya vyoo 2369, katika shule za msingi pia kwa upande wa Sekondari Zaidi ya billion 18 zimetumika kujenga madarasa 327, nyumba za walimu 37, matundu ya vyoo 474, mabweni 27, Hosteli 13, Maabara 128, maktaba 4, bwalo za chakula 8, majengo ya utawala 2, na ukarabati wa shule kongwe 4 katika shule za Sekondari.
Aidha baada ya hotuba yake aliomba kura kwa wananchi kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ( Rais, Mbunge, na Madiwani) ili waweze kuleta maendeleo ndani ya jimbo la Songea.
Mwisho alichukua ilani ya utekelezaji ya CCM na kumkabidhi mgombea Ubunge wa Jimbo la Songea mjini Dr. Damas Ndumbaro ili aweze kuisimamia na kutekeleza kwa ajili ya wananchi wa Tanzania.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY, AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
16.09.2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa