Machinjio hii ikikamilika wekeni mifumo mizuri na salama ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri yetu kwasababu, TAMISEMI imeanzisha miradi hii ili Halmashauri zetu ziweze kukusanya mapato.
Kauli hiyo imetemkwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Said Jafo akiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya miundombinu ya Barabara, ujenzi wa machinjio Mpya ya kisasa, pamoja na kituo cha stendi cha mabasi Tanga na kisha alifanya mkutano na watumishi wa Manispaa Songea leo tarehe 23 disemba 2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mh.Jafo alianza kuipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara km 10.3 ambazo zimejengwa kwa kiwango kizuri cha Rami kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu ya mifereji na taa. Amewataka wananchi kuendelea kuzitunza barabara hizo na kutoruhusu kutupia takataka.
Manispaa ya Songea na Halmashauri nyingine zinaingizwa katika miradi mingine ya miji 45 na kufanya uboreshaji mkubwa wa miundombinu ya Barabara. Mpango wa Serikali katika Miji 45 utakuja kufanya kazi nyingine kubwa katika Manispaa ya Songea. Kwa hilo ondoeni shaka. Alisema Mh. Jafo.
Aliongeza kuwa uwekezaji huu utasaidia Halmashauri kupata mapato makubwa Zaidi pamoja na kutanua uwigo wa biashara kwa utoaji wa nyama bora kwenda Nchi nyingine za jirani.
Akimpongeza Kaimu Mhandisi Manispaa ya Songea Caroline M. Bernard kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa barabara, machinjio mpya ya kisasa, na stendi ya mabasi Tanga, ambapo alibainisha kuwa kutokana na kuridhishwa na utendaji wake alishauri angepandishwa daraja na kuwa mkuu wa Idara.
Amewataka viongozi na wataalamu kufanya kazi kwa ushirikiano wa kukusanya mapato ya Serikali kwa kuacha migogoro isiyo na tija ndani ya Halmashauri ili kukusanya mapato hayo kufikia 50% kila Halmashauri ifikapo januari 15 2021. Alisema hakuna mtu aliyetulazimisha katika upangaji wa bajeti, na ikiwa bajet tumeipanga wenyewe, mipango ya kwetu wenyewe, hakuna sababu ya kufeli kukusanya mapato. “alisisitiza mh. Jafo.”
Aidha, katika utoaji wa mikopo ya 10% inayosimamiwa na maendeleo ya jamii kwa kupitia vikundi vya vijana 4%, wanawake 4% na walemavu 2% inatakiwa kutoa kipaumbele kwa vikundi vya wajasiliamali ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa yenye riba nafuu na Serikali kwa lengo la kukuza mitaji yao.
Alisema “ nanukuu “ Kumbukeni hotuba ya Mh. Rais ya novemba 20 mwaka 2015, wakati anazindua Bunge la 15, ukiachilia agenda ya ufisadi na wizi, jambo jingine ni uzembe uliopitiliza kwa watumishi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa , alikuwa hapendezwi kabisa na utendaji wa kazi, uzembe wa ukusanyaji mapato, na miradi isiyokizi kiwango.” Mwisho wa kunukuu”
Naye Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Songea Caroline M. Bernard alisema Mradi wa ujenzi wa machinjio kwa awamu ya kwanza umegharimu 2,748,850,900.00 ambapo kwa awamu ya pili mradi wa machinjio ulianza kutekelezwa tarehe 11 januari 2020 na unatarajiwa kukamilka 30 disemba 2020 na hadi kukamilika utagharimu 5,748,799,559.00.
Caroline alibainisha kuwa mradi wa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi Tanga ulianza kutekelezwa tarehe 25.03.2018 na umekamilika tarehe 12.02.2020 kwa gharama ya shilingi 6,887,083,722.60. Mh. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Katika kikao cha ufunguzi wa baraza la madiwani kilichofanyika 16 disemba 2020 aliliagiza baraza la madiwani kuhakikisha kituo hicho cha mabasi kinafanya kazi kwa ufanisi kuanzia 01 januari 2021.
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Leodgar Mbano alisema kupitia agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa katika Mkutano wa baraza la Madiwani wameanza kutekeleza leo 23 disemba kwa kuitisha kikao cha wadau ili waweze kutekeleza agizo hilo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
23 disemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa