Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe. Michael Mbano, amewataka wataalamu wa manispaa kuhakikisha wanatekeleza miradi mbalimbali kwa ufanisi na kwa wakati.
Mhe. Mbano amesisitiza umuhimu wa kusimamia miradi ya maendeleo kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Amefafanua kwamba fedha tayari zimeshawasili katika baadhi ya kata kwa ajili ya miradi hiyo, huku akitoa rai kwa kitengo cha Manunuzi kuhakikisha wanatekeleza taratibu bila kukwama kwa sababu ya Mfumo wa Manunuzi (NEST).
Aidha, Mhe. Mbano alieleza shukrani zake kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwekeza fedha katika miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Songea.
Haya yalijiri wakati wa kikao kazi cha Baraza la Madiwani, kilichohusisha madiwani wa kata zote 21, maafisa watendaji, wakuu wa idara, na vitengo, ambapo walijadili taarifa kutoka katika kata. Kikao hicho kilifanyika siku moja kabla ya Mkutano wa Baraza la Madiwani.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa