Diwani wa kata ya Matogoro Issa S.Mkwawa amefanya tafrija fupi ya kuwapongeza walimu wote wa shule zilizopo katika kata Ya Matogoro kwa kufaulisha mtihani wa darasa la saba pamoja na mtihani wa kidato cha nne 2020.
Mkwawa ametoa pongezi hizo kwa shule za Msingi tatu na Sekondari 2,( Shule ya Msingi Matogoro, Shule ya Msingi Chemchem, Shule ya Msingi Mahilo, Kalembo Sekondari, na Matogoro Sekondari) kwa lengo la kuwatia moyo Walimu ambao wamefaulisha vizuri masomo yao ili waweze kuongeza bidii katika kutekeleza wajibu wao. Tafrija hiyo ilifanyika tarehe 05/03/2021 katika ukumbi wa chuo cha walimu songea.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa nipamoja na sukari kilo 10 kwa kila shule, fedha shilingi 40,000/= kwa kila mwalimu aliyefaulisha vizuri katika masomo, zawadi kwa wanafunzi waliofaulu daraja la kwanza,na la pili pamoja na fedha shilingi 1,200,000 zimetolewa kwa ajili kulipa walimu wawili wa wahesabu watakao jitolea kufundisha hesabu kwa muda wa miezi sita kwa sekondari ya Kalembo na Matogoro.
Alisema baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa walimu wa hisabati wakati Serikali ikifanya utaratibu wa kutatua changamoto hiyo, Kiongozi huyo makini aliamua kulipa kiasi hicho cha fedha shilingi laki sita kila sekondari kwa ajili ya malipo ya mwalimu atakayejitolea kufundisha wanafunzi shule ya kalembo na matogoro.
Aliongeza kuwa kilichomvutia ni kuona shule za kata zinafanya vizuri kwa baadhi ya wanafunzi kfaulu dalaja la juu hatimaye kushika nafasi ya 18 na 19 Kiwilaya kati ya shule 36 zilizofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2020.
Alibainisha kuwa Kata ya Matogoro imejipanga vizuri katika kutekeleza ILANI ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuanza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo na miundombinu ya shule, vivuko, zahanati na majengo ya kiutawala kwa kuwashirikisha wananchi/wadau mbalimbali ili kufikia malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuweka mpango shirikishi jamii kwa wananchi wenyewe wa kuibua miradi kipaumbele.
Mkwawa alisema hadi hivi sasa kata hiyo imeshajenga nyumba ya Mganga moja ambayo ipo hatua ya ukamilishaji ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi katika Zahanati ya Mahilo, pamoja na ujenzi wa ofisi ya Mtaa Mkwawa ambayo ipo hatua ya Renta ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi.
Alitoa rai kwa wananchi, wazazi na kamati za shule kuendelea kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuleta maendeleo mazuri ya wananfunzi. Ameahidi kuendelea kutoa zawadi kwa shule zake zote ndani ya kata hiyo kila mwaka ili kuwatia moyo walimu kwa kufanya kazi vizuri.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
08 MACHI 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa