Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Mwinyi Msolomi ameongoza mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi kilichofanyika tarehe 16 februari 2025 katika ukumbi wa CCM Songea uliofanyika kwa lengo la kusoma Ilani ya chama hicho kwa muda wa miaka miwili tangu waingie madarakani.
Akizungumza Mwenyekiti wa chama hicho amewataka wanachama hao kutekeleza maagizo yaliyotolewa kupitia mkutano mkuu ccm Taifa ambayo kila mmoja wao anapaswa kumsemea Dkt. Samia Suluhu Hassan Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka nne tangu aingie madarakani.
Amewataka kujenga mahusiano ili kazi ziweze kufanyika sambamba na kuwakumbusha wajumbe hao wajibu na maadili ya utendaji kazi bila kuleta mkanganyiko na amewatahadharisha kutoweka makundi ya kisiasa ambazao zitawagawa kwenye makundi kuelekea kipindi cha uchaguzi.
Kwa upande wake katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Komredi James Mgego amesema katika kipindi cha miaka miwili ya viongozi wa CCM Wilaya wameweza kutekeleza shughuli mbalimbali hususani miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa, idadi ya usajili wa wanachama wapya, idadi ya vikao vilivyofanyika ndani ya chama, pamoja na ujio wa viongozi.
MWISHO.
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa