Maadhimisho ya miaka 23 ya kuanzishwa kwa kituo cha Afya Mjimwema yamefanyika tarehe 11 Oktoba 2024 ambayo yameazimishwa kwa mara ya kwanza kwa lengo la kufanya kumbukizi ya wapi walipotoka na wapi wanakoelekea.
Maadhimisho hayo yamefanyika kata ya Mjimwema ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Sylivester Mhagama Diwani wa Kata ya Mjimwema kwa lengo la kufanya tahimini ya maendeleo na kubaini changamoto za kituoni hapo ambazo hujitokeza katika kituo hicho.
Mhe. Mhagama akifafanua namna ya kutatua changamoto kituoni hapo alisema, pamoja na kuendelea kutenga bajeti ya kujenga miundombinu mbalimbali ya kituo cha afya Mjimwema lakini ipo haja ya kuwashirikisha Wananchi kuchangia ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo na WODI ya wanaume ambayo inahitajika kituoni hapo.
Hatua za awali za utatuzi wa changamoto hizo Mhe. Aliongoza arambee ya kuchangia maendeleo ambapo waliweza kuchangia tsh Milioni 2,525,0000 ambazo zimechangwa kwa ajili ya hatua ya awali ya uchangiaji wa maendeleo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa