Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Bil. 9 kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya Elimu Msingi na Sekondari katika kipindi cha miaka miwili 2021 hadi 2023 katika Manispaa ya Songea.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepata mafanikio makubwa kupitia Sekta ya Elimu ambapo imesaidia kupunguza changamoto ya madarasa 142 pamoja na madawati au viti na meza sambamba na utoaji wa elimu BURE kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita. TUNASHUKURU.
Hayo yamejilii katika kikao cha waandishi wa Habari kilichofanyika leo tarehe 17 machi 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kutoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mafanikio ya utekelezaji wa miaka miwili ya Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kimeongozwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano ambaye amesema” katika kipindi cha awali Manispaa ya Songea ilikuwa na vituo vya afya viwili ambapo mara baada ya uongozi wa awamu ya sita Manispaa ya Songea imejenga vituo vya afya vinne ikiwemo na kituo cha afya Lilambo kilichojengwa kwa mapato ya ndani, kituo cha afya Mletele, kituo cha afya Subira na kituo cha afya Msamala kwa gharama ya Bil. 3.550. ‘Alipongeza”
Mhe. Mbano aliongeza kuwa katika Sekta ya kilimo kwa mwaka 2022/2023 Manispaa ya Songea imefanikiwa kupokea Pembejeo ya RUZUKU Tan 15,487 kwa wakulima 137,487 ambapo ongezeko hilo limetokana na Serikali kuweka Ruzuku ya Mbolea kwa Mkulima.
Akizungumzia kuhusu Sekta ya Barabara katika Manispaa ya Songea ilipokea kiasi cha Bil. 6.133 kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu ya barabara, madaraja na mifereji hususani katika barabara ya Lami Kata ya Seedfarm, Lizaboni, kata ya Bombambili Sanga one hadi Ujenzi. “Alibainisha.”
Aidha, Bil. 1.2 zimetolewa na Halmashauri kwa ajili ya kuvikopesha vikundi mbalimbali vya wajasiliamali wadogo kwa wanufaika wa vikundi vya wanawake 4%, Vijana 4% na walemavu 2% fedha hizo ni mafanikio ya makusanyo ya mapato ya ndani ya 10% pamoja na Kaya 5611 zimenufaika na Mfuko wa TASAF kwa watu wasioweza kujikimu ili kuondoa umaskini katika kaya kwa ujumla..
Katika kutekeleza shughuli za Mpango na Mikakati ya kimaendeleo Serikali imefanikiwa kusimamia zoezi la SENSA ya Watu na Makazi na POSTI KODI ambapo kwa Manispaa ya Songea ina jumla ya wakazi 286,285 hii itasaidia kupanga mipango ya maendeleo ikiwemo na kufahamu mahitaji halisi ya kijamii.
Alipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kutoa fedha Zaidi ya Bil. 145 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa miji 28 kwa ajili ya kumtua mama ndoo kichwani ambapo kwa Manispaa ya Songea itawezesha kuondoa kero ya maji kwa asilimia 95%. “Mhe. Mbano Aliongeza”.
Aliongeza kuwa Manispaa ya Songea inatarajia kuanza utekelezaji wa miradi ya Masoko mawili ya kisasa Manzese A na Manzese B, pamoja na ujenzi wa kiwango cha Lami KM 10.5 ambao Unatarajia kujengwa hivi karibuni pamoja na ujenzi wa chuo kikuu cha Uhasibu Arusha katika Kata ya Tanga.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa