Milion 418,436,332/= za daiwa kutorejeshwa mkopo wa vikundi vya wanawake 4%, vijana 4%, na walemavu 2% sawa na asilimia 10%, fedha ambazo kama zingerejeshwa kutoka kwenye vikundi hivyo zingeweza kukopeshwa kwa wanavikundi wengine.
Kauli hiyo imetamkwa na katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Daniel katika mafunzo yaliyofanyika tarehe 30 disemba 2020 katika ukumbi wa manispaa ya Songea kwa lengo la kuidhinisha utoaji wa mikopo kwa wanavikundi 52 ikiwa wanawake vikundi 26, vijana vikundi 20 na walemavu vikundi 6.
Pendo, alitoa pongezi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kutoa mikopo kwa wanavikundi kiasi cha shilingi 108,669,444.08 kwa mwezi disemba kwani sio kila Halmashauri inauwezo wa kutoa mikopo hiyo kwa wanavikundi.
Amewataka wanavikundi wote wanaodaiwa mkopo huo kufanya marejesho ya fedha 418,436,332/= walizokopa ambazo bado hazijarejeshwa, endapo hawatarejesha fedha hizo, watachukuliwa hatua za kisheria.
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema tumeanza kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuanza kutoa mikopo kwa wanavikundi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha 2025.
Mbano ametoa rai kwa wanavikundi hao kutekeleza makubaliano yao kadili ya maandiko waliyokubaliana ikiwemo na kufanya marejesho ya mkopo kwa wakati ili waweze kukopeshwa wanavikundi wengine.
Alieza bayana kuwa “ Serikali hii haipendi udanganyifu, uongo, na utapeli na endapo utachukua fedha za Serikali ambayo imekusaidia kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine lakini hutekelezi kwa maksudi jukumu lako la kulipa deni basi hauna tofauti ya mwizi yeyote yule.” Alisisitiza Mbano.
Naye kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Songea Mensa Ngelangela katika hotuba yake iliyosomwa kwa mgeni Rasmi alibainisha kuwa mwezi disemba 2020 mikopo iliyotolewa kwa wanavikundi wanawake 4% kiasi cha 16,000,000/=, vikundi vya vijana kiasi cha 16,000,000/= na vikundi vya walemavu kiasi cha 8,000,000/=.
Mensa aliongeza kuwa fedha za marejesho zikiwa na mgawanyo wa asilimia 4% wanawake shilingi 12,000,000 na asilimia 4% vijana 12,000,000 na 20% watu wenye ulemavu 6,000,000 pamoja na bakaa zikiwa na mgawanyo wa 4% wanawake shilingi 15,467,777.912, asilimia 4% vijana shilingi 15,467,777.912 na walemavu shilingi 7,733,883.96.
Katika kutatua changamoto za wadaiwa wa mkopo, Idara ya maendeleo ya jamii imeweka mikakati ya kufanya uhakiki wa vikundi vyote vinavyoomba mkopo, kabla ya kupewa mkopo huo watatakiwa kwenda kukagua miradi yao ili kujiridhisha na vikundi hivyo.
Naye Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Songea Amos Lugomela alisema kazi yao ni kuchunguza na kushauri namna ya kuzuia mianya ya rushwa, na wale wote wanaochunguzwa, ushahidi ukipatikana wanafikishwa mahakamani ili waweze kujibu mashitaka yanayowakabili.
Lugomela alisema kwa mujibu wa semina hiyo ya utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali alibainisha kuwa Serikali za mitaa zote kisheria zinapaswa kutenga 10% kawajili ya vikundi vya wanawake 4%, vijana 4%, na walemavu 2%, hiyo ni kwasababu ya kuleta maendeleo kwa wanannchi wake.
Ametoa rai kwa wale wote waliokopa mikopo hiyo na hawajarejesha mikopo yao ambayo ni jumla ya shilingi milioni 418,436,332 ambazo zindaiwa kutorejeshwa na wanavikundi, walipe mara moja na endapo hawatarejesha fedha hizo watachukuliwa hatua za kisheria.
Amewataka Maafisa Maendeleo ya jamii baada ya kutolewa mikopo hiyo kwa wanavikundi watatakiwa kupeleka majina ya wanavikundi waliokopa sasa na wadaiwa wote yakionyesha mahali wanapoishi na shughuli wanazozifanya ili waweze kufuatiliwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
31 disemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa