Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amewaasa Wajasiliamali wadogo kutumia mikopo yao Vizuri ili kuinua mitaji ya Biashara zao pamoja na kukuza kipato.
Pololet amesema hayo katika kikao cha Wanavikundi Wajasiliamali Wanawake, Vijana, pamoja na Makundi Maalum katika zoezi la Ugawaji wa Mikopo kwa Vikundi 26 kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea leo 08/06/2020.
Alisema”Lengo la kugawa Mikopo Tsh 45 mil kwa Wanavikundi ni kuwajengea Uwezo wa kufanya shughuli za Ujasilimali na kuinua kipato cha jamii ya Manispaa ya Songea. Aliongeza kuwa Mkopo huo ni Fedha Asilimia 10% ya Makusanyo ya mapato ya ndani kwa mchanganuo wa 4% Wanawake, 4% Vijana, 2% makundi maalum.”
Awali fedha hizo zilikuwa zikitolewa kila baada ya miezi mitatu, lakini kuanzia sasa Manispaa ya Songea itaendelea kutoa Mikopo kwa wanavikundi kila Mwezi, hivyo nilazima zirudishwe fedha hizo kwa wakati ili waweze kukopeshwa wanavikundi wengine wenye sifa.
Alifafanua kuwa” Mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa Vikundi haina Riba, Hivyo mnapaswa kufanya marejesho kwa wakati ili muwezez kukopeshwa tena. Alisema hatutaki Wajasiliamali ambao hawabadiliki kiuchumi bali tunahitaji Wajasiliamali ambao wataleta mabadiliko Kiuchumi.” Alisisitiza.
Alisema Mikopo kwa Vikundi ni Bora kuliko Mkopo wa mtu mmoja mmoja kwasababu vikundi husaidia kushirikiana kimawazo, kupeana uzoefu na kujenga uaminifu.
Naye Mkurugenzi Manispaa ya Songea Tina Sekambo akiwakilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Songea Judith Ngowe alisema “ Chanagamoto kubwa inatokana na baadhi ya wanakikundi kutorejesha Mikopo kwa wakati. Hata hivyo, alibainisha baadhi ya mikakati waliyojiwekea ili kukabiliana na changamoto hiyo ni pamaoja na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wasiorejesha Mikopo hiyo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa