Komredi Oddo Mwisho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma amewataka viongozi na Wataalamu Manispaa ya Songea kulinda rasilimali za shule ili miundombinu ya shule hizo iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
Alisema Manispaa ya songea imekuwa ikiendeleza rekodi nzuri ya kujenga miundombinu ya Afya na Elimu kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ambapo kwa mwaka 2022 Manispaa ya Songea walijenga kituo cha Afya kata ya Lilambo kwa gharama ya Mil 500 ambacho kimeanza kutoa huduma.
Aidha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Manispaa ya Songea imeweza kujenga Shule mpya ya mchepuo wa kiingereza kwa gharama ya Mil. 500 ambayo inatarajia kukamilika ifikapo mwezi Novemba 2023 na kupokea wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2024.
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika tarehe 08 Oktoba 2023 ambayo waliweza kukagua na kutembelea jumla ya miradi mitano 5 yenye thamani ya shilingi 2,791387,467.00 ambapo kiasi cha 2,291,387,467.00 ni fedha za serikali kuu na kiasi cha 500,0000,0000.00 ni fedha za mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Mletele ambacho kilipokea fedha kiasi cha Shilingi 545,334,640.00 kutoka Global Fund ambapo Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, ujenzi wa shule ya Lawrance Gama kwa thamani ya Mil. 560,552,827/= ambao ni miongoni mwa shule zilizonufaika na mradi wa Uimarishajaji wa Miundombinu ya Elimu Sekondari (SEQUIP) ambao upo hatua ya 60%.
Aidha, miradi mingine ni ujenzi wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza Chifu Zulu (Chief Zulu Academy) inayojengwa kwa gharama ya Mil. 500 fedha za mapato ya ndani iliyopo kata ya Mshangano ambao utakijikita katika tekinolojia ya tarakinishi (Computer Technology) ambayo imelenga kuwasaidia watoto na wazazi wanaohitaji huduma ya shule bora zenye mfumo kwa gharama nafuu.
Ujenzi wa madarasa manne, na mabweni mawili 2 katika shukle ya wasichana Songea kwa gharama ya Mil. 280,000,000.00 fedha za mradi wa SEQUIP 2022, pamoja na ujenzi wa madarasa 10, mabweni 4, na matundu 15 katika sekondari ya Emmanuel Nchimbi kwa kiasi cha Tsh Mil 905,500,000 fedha kutoka Serikali kuu.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea alisema baraza la Madiwani walitenga bajeti ya Mil. 500 kwa ajili ya kujenga shule ya mchepuo wa kiingereza ambayo itaendeshwa kwa gharama nafuu na itawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri.
Imeandaliwa na
AMINA PILLY,
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI - SONGEA MC
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa