MILANGO ya utalii mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma inaendelea kufunguka ambapo sasa serikali inatarajia kuanzisha bustani ya wanyamapori katika Milima miwili na visiwa viwili vilivyopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Afisa wa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema mchakato wa kuendeleza Hifadhi ya mlima Mbamba(Mbamba hill) iliyopo mjini Mbambabay na hifadhi ya mlima Tumbi iliyopo kijiji cha Ndengere ni maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe ambaye aliagiza Nyasa iwe kitovu cha utalii kusini.
Challe anabainisha kuwa Mbamba Hill imeunganishwa na kisiwa kinachoitwa Zambia ambacho kipo meta 300 toka ufukweni mwa ziwa Nyasa na kwamba kisiwa hicho kina utajiri wa samaki wa mapambo ambao ni kivutio cha watalii.
Anasema Mbamba Hill tayari imepimwa na kubainika ina ukubwa wa hekta 420 na kwamba bajeti ya kujenga uzio kuzunguka Mbambabay Hill imepitishwa na kwamba ujenzi unatarajia kuanza wakati wowote fedha zitakapoletwa na kwamba mara baada ya ujenzi wa uzio kukamilika wanyamapori wa aina mbalimbali wanatarajia kuwekwa.Challe anasema mara baada ya kukamilisha mradi wa hifadhi wa Mbambabay na kisiwa cha zambia,mradi utakaofuata ni mlima wa hifadhi wa Tumbi,uliopo kijiji cha Ndengere ambao utaunganishwa na kisiwa cha Lundo chenye ukubwa wa kilometa za mraba 20 hivyo kuwa na hifadhi mbili ambazo zimeunganishwa na visiwa viwili.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa