MILIMA YA MATOGORO:CHANZO CHA MITO MITATU MAARUFU
MILIMA ya Matogoro iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,ni kivutio adimu katika Manispaa hiyo kwa kuwa milima hiyo yenye misitu ya asili na ya kupandwa ndiyo chanzo cha mito mitatu maarufu nchini.
Mto wa kwanza ambao chanzo chake ni milima hiyo ni mto Ruvuma ambao ni maarufu barani Afrika ambao unamwaga maji yake Bahari ya Hindi lakini pia mto huo unaunganisha nchi za Tanzania na Msumbiji.
Milima hiyo pia ni chanzo cha Mto Luhira ambao unatengeneza mto Ruhuhu unaomwaga maji yake ziwa Nyasa.Mto Ruhuhu unachangia asilimia 20 ya maji katika ziwa Nyasa.
Mto wa tatu ambao unaanzia katika milima hiyo ni mto Luegu ambao unaungana na mto Rufiji unaomwaga maji yake Bahari ya Hindi.
Hifadhi ya Msitu wa milima ya Matogoro ilianzishwa miaka ya 1950 ikiwa na hekari 2259 za miti ya kupandwa.Msitu wa milima ya Matogoro kisheria upo chini ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na ulitangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka 1951.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa