Manispaa ya Songea imetoa kiasi cha Tshs 113, 760, 000/= kwa jumla ya Vikundi vya wajasiliamali 48 vyenye wanachama 144 ikiwa vikundi vya wanawake 39, vikundi vya vijana 07 na vikundi vya watu wenye ulemavu 2.
Mikopo hiyo imetolewa ikiwa ni makusanyo ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani ambapo wanawake asilimia 40%, vijana 40% na walemavu asilimia 20%, tukio hilo limefanyika leo tarehe 29 Juni 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea, kwa lengo la kuwainua wajasiliamali wadogo waliopo katika Manispaa ya Songea.
Mgeni rasmi katika zoezi hilo la utoaji wa mikopo kwa vikundi 48 alikuwa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Utalii na Maliasili ambaye aliwakilishwa na Naibu Meya Jeremia Mlembe ambapo aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuonyesha juhudi katika kutekelezaji wa sheria na kanuni za uchangiaji wa 10% ya mapato ya ndani pamoja na uhimizaji wa utoaji wa mikopo ambapo kiasi cha Tshs. 113,760,000/= zimetolewa.
Jeremiah alisema Mkopo huu utumike kwa ajili ya miradi yenu kulingana na maandiko ya miradi iliyoombwa ili iweze kuleta Mafanikio ya haraka kwa jamii sambamba na kufanya marejesho mkopo kila mwezi na kwa wakati ili kuwapatia fursa wahitaji wengine kukopeshwa na endapo hawatarejesha kwa wakati watachukuliwa hatua za kisheria. ’Alisisitiza’
Amewata wajasiliamali hao kujitokeza kwenda kupima afya kwa hiari, kujilinda na janga la UKIMWI pamoja na CORONA.’ Jeremia alieleza’
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea Martin Mtani amesema kabla ya kutoa mkopo huo timu ya wataalamu ilifanya ufuatiliaji na uhakiki kwa vikundi vyote vilivyoomba mikopo na baadhi ya miradi ya vikundi vilivyokidhi vigezo ni ufugaji wa kuku, nguruwe, ushonaji, ufumaji wa makapu na utengenezaji batiki.
Mtani aliongeza kuwa utoaji wa mikopo hiyo umewasaidia wanufaika wengi kuweza kuboresha makazi yao, kusomesha watoto na kutoa ajira kwa watu wengine.
Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatarajia kuboresha utaratibu wa utoaji wa mikopo mikubwa kwa vikundi vyenye miradi yenye tija ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’Alibainisha’
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA,
29.06.2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa