Hayo yamebainika katika ziara ya Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni Dr Harrison Mwakyembe iliyofanyika 12-13/08/2020 Manispaa ya Songea.
Mwakyembe alisema lengo la ziara ni kutembelea kituo cha Redio TBC Taifa kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa usikivu wa Redio ya Serikali na kubaini kama kuna changamoto ambazo zinakwamisha utandaji bora wa Mitambo hiyo ambapo aliweza kutembelea Mitambo ya TBC Taifa iliyopo katika milima ya Matogoro, kituo cha Redio Jogoo,na Key FM pamoja na maeneo ya urithi wa ukombozi yaani makumbusho ya Majimaji MKoani Ruvuma.
Awali TBC Taifa ilikuwa na changamoto ya usikivu kwa baadhi ya maeneo Mkoani Ruvuma lakini kupitia mitambo iliyowekwa Matogoro imesaidia kuondoa tatizo hilo ambapo kwasasa TBC Taifa inasikika vizuri bila tatizo lolote.
Hakusita kuwapongeza wamiliki wa Redio zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea Key FM, na Jogoo FM kwa uwekezaji mzuri ambao pia wamesaidia kutoa ajira kwa jamii pamoja na kuliongezea pato Taifa letu (Kodi).
Alibainisha kuwa taalma ya uandishi wa habari ni taalma muhimu ambayo huzingatia sheria, kanuni na maadili katka kuichakata habari kitaalamu na kuitoa kwa jamii bila kukiuka miiko ya taalma hiyo. Pia aliongeza kuwa mwandishi wa habari ni Mwalimu, Mchambuzi wa habari, hufanya kazi ya kutafuta habari na kuripoti kitu chochote kilichotokea katika jamii.
Akizungumzia kuhusu michezo, alisema ni muhimu sana kuibua vipaji vya watoto wazawa ili kuwaandaa kimichezo hapo baadae na hatimaye tutaweza kuachana na dhana ya kuwategemea wachezaji wa kigeni ambao vipaji vyao ni vya kawaida. Alisistiza.
Aliongeza kuwa msimu ujao wa michezo atahitaji kuona kwamba mchezaji wa nje yeyote atakayesajiliwa kucheza Tanzania atatakiwa kuwa na sifa thabiti na awe anacheza ligi kuu kwao au timu ya Taifa lake, au awe anahistoria ya kucheza kwenye timu zilizopo kati ya 50 bora.
Alisema amepokea changamoto ya uhaba wa maafisa michezo Mkoani Ruvuma ambapo alisema ni Halmashauri Tunduru pekee yenye Afisa michezo kati ya Halmashauri nane zilizopo Mkoani Ruvuma, na ameahidi kulifanyia kazi.
Naye Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji Mkoa wa Ruvuma Adson Ndyanabo alisema” nanukuu” Makumbusho ya Taifa la Tanzania inapenda kuishukuru Serikali ya awamu ya tano (5) chini ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwakutupatia Zaidi ya Tshs 164,000,000/= kwa ajili ya ukarabati wa Makumbusho ya Dkt. Kawawa kazi inayosimamiwa na wakala wa majaengo (TBA) kwa ajili ya kuboresha miundombinu.”mwisho wa kunukuu.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI –MANISPAA YA SONGEA.
14.08.2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa