JUMLA ya shilingi milioni 22 zimetumika kwa ajili ya kukamilisha maabara katika shule ya sekondari ya Matogoro iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mkuu wa shule hiyo Ezra Mwogela amebainisha kuwa kati ya fedha hizo,shilingi milioni 17 zimetumika kwa utengenezaji na uwekaji wa samani za maabara na shilingi milioni tano zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa maabara.
Amezitaja shughuli ambazo zimefanyika kwa shilingi milioni 17 kuwa ni kutengeenza meza 16 za wanafunzi,kutengeneza meza mbili za nyuma(back table),kutengeneza stuli 50 za maabara na kuweka mfumo wa maji safi na taka.
Kazi nyingne zilizofanyika kwa mujibu wa Mwogela ni kuingiza umeme katika maabara,kusakafia mfereji wa maji safi na maji taka,kutengeneza vifuniko vya mifereji ya maji safi na taka na kuchimba na kujenga shimo la maji safi na taka.
“Shilingi milioni zimetumika kuweka jipsum vyumba viwili vya maabara,kupaka rangi katika vyumba viwili vya maabara,kufunga shata vyumba viwili vya maabara,kumalizia ujenzi wa chumba cha ofisi ya maabara,kusakafia na kupiga lipu chumba cha ofisi ya maabara,kutengeneza grili za milango na kutengeneza ngazi maalu kwa wenye ulemavu’’,anasema Mwogela.
Kulingana na Mkuu huyo wa shule,kazi ya ujenzi wa maabara imefanyika kwa asilimia 98 ambapo amemshukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya maabara ya shule hiyo.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manipaa ya Songea
Juni 28,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa