KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 Charles Kabeho amefungua vyumba vinne vya madarasa katika shule ya Msingi Kibulang'oma iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Kabeho amefungua vyumba hivyo vya madarasa baada ya kufanya ukaguzi na kuridhika na viwango vya ujenzi katika shule hiyo.
Shule ya msingi Kibulang’oma ni miongoni mwa shule za msingi zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea zinazomilikiwa na Halmashauri. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 965 wakiwepo wakike 508 na wakiume 457.Lengo la mradi huu ni kupunguza msongamano wa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kusomea.
Mradi huu una jumla ya madarasa manne yenye jumla ya madawati 60 ambapo kila lina madawati 15. Mradi huu mpaka sasa umegharimu zaidi ya shilingi milioni 37 na kwamba ni matarajio ya mradi huo utapunguza tatizo la msongamano wa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kusomea wanafunzi.
Wazazi na walezi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo wameishukuru serikali na Viongozi wa kata ya Lizaboni, Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Serikali kuu na Mhisani katika kuchangia Ujenzi wa Vyumba ambavyo vimekamilika na vinaanza kutumika rasmi baada ya kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 11,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa