NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
26.10.2021
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amepokea fedha za mpango wa maendeleo ya Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambazo ni kiasi cha Milioni 660,000,000.
Fedha hizo zimetolewa kutoka Serikali kuu chini ya uongozi wa Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Songea.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa vyumba 26 vya madarasa katika shule za Sekondari kiasi cha shilingi 520,000,000, ujenzi wa vymba vitatu vya madarasa katika vituo shikizi vya shule ya msingi Nonga nonga kiasi cha shilingi 60,000,000, ujenzi wa bweni moja la wanafunzi katika shule ya msingi Ruila yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu kiasi cha shilingi 80,000,000.
‘KAZI IENDELEE’ .
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa