Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
08.02.2022
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amefanya ziara kutembelea miradi ya maendeleo tarehe 07 februari 2022 inayotekelezwa kwa fedha za tozo zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea fedha za Tozo shilingi million 300 ambazo zitatumika kwajili ya ujenzi wa kituo cha afya Subira kwa gharama ya Tsh Mil 250 pia shilingi milioni 50,000,000 zimetumika kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa 4 manne kwa gharama ya shilingi million 12,500,000 kwa kila darasa moja.
Dkt. Sagamiko aliongeza kuwa kupitia mapato ya fedha za ndani Manispaa ya Songea imetenga bajeti ya fedha shilingi million 500,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Lilambo ambacho kipo hatua ya lipu sambamba na utekelezaji wa mpango mkakati wa ujenzi wa hospitali ya Manispaa ambayo itajengwa katika eneo la Shule ya Tanga Manispaa ya Songea.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa