MWENGE wa Uhuru 2024 ukiwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea umepita katika tarafa 2, kata 13, Mitaa 39 na umekimbizwa umbali wa KM 98.2 ambapo umepita katika miradi 9 ikiwemo na kuweka jiwe la msingi katika miradi miwili, ugawaji wa vifaa katika mradi mmoja, na kutembelea miradi 6 yenye jumla ya Shilingi Bil. 25, 193,941,237.30.
Hayo yamejiri wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba ambapo Mwenge wa Uhuru uliwasili Manispaa ya Songea tarehe 14 Juni 2024 na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile ukitokea Wilaya ya Mbinga.
Kiongozi waMbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzani mazingira na kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kutunza amani katika maeneo yote hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Malaria, ukimwi, Rushwa pia amesisitiza Lishe bora na siyo kujaza tumbo.
Akitoa taarifa ya miradi mbalimbali kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Wakili. Bashir Muhoja amesema” Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 12 zilizobahatika kupata miradi wa ubaoreshaji wa miundombinu ya barabara za lami nzito zenye urefu wa KM 10.1 yenye jumla ya barabara 20 za lami katikati ya Mji wa Songea wenye thamani ya zaidi ya Bil. 22 ambao umefadhiliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya kimataifa (IDA) kupitia Benki ya Dunia kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na ushindani wa Miji, Manispaa, Majiji Nchini Tanzania (TACTIC) ambao unaratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambao umefikia asilimia 20 ya utekelezaji wa barabara hiyo.
Aidha miradi mingine iliyotembelewa na mwenge wa uhuru ni mradi wa maji katika kata ya Tanga Mtaa wa Pambazuko Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambao umegharimu shilingi 778,149,730 unaotarajia kuhudumia watu 15,990.
Miradi miwili iliyowekwa jiwe la Msingi ni ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi unaogharimu Shilingi Mil. 180 hadi utakapokamilika, pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 na matundu 10 ya vyoo yenyejuml ya thamani ya Mil. 259,500,000 katika shule ya Sekondari Londoni ambapo shule hiyo ilianzishwa mnamo 2004 ina wanafunzi wanaosoma kidato cha kwanza hadi kidato cha sita wapatao 1,399 pia kukamilika kwa mradi wa vyumba 10 vya madarasa utawezesha kurahisisha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa