UJENZI wa kituo kikuu cha mabasi unafanyika katika eneo lenye ukubwa wa hekari 15 lilipo katika Kata ya Tanga kilomita 12 toka katikati ya Manispaa ya Songea. Ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi Songea, ulianza tarehe 25/03/2018 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30/09/2019. Ujenzi unafanywa na Mkandarasi CHINA SICHUAN INTERNATIONAL CORPORATION (SIETCO) na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri BUREAU FOR INDUSTRIAL CORPORATION (BICO) ambao ni Chuo kikuu cha Dar –es- salaam. Mpaka sasa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 82 ya utekelezaji
Mradi huu mpaka kukamilika utagharimu jumla ya Tshs 6,189,340,930. Mpaka sasa Mkandarasi amelipwa kiasi cha Tshs 2,736,965,106.20 ikiwa ni pamoja na malipo ya awali (Advance payment). Gharama za Mhandisi mshauri ni 319,571,801.60 kati ya fedha hizo amelipwa Tshs 180,748,637.51
Mradi mwingine ambao unatekelezwa ni Ujenzi wa barabara km 10.3 kiwango cha lami nzito. Ujenzi wa barabara hizi ulianza tarehe 01/07/2015 na ulitakiwa kukamilika tarehe 30/06/2017. Mradi huu umetekelezwa na Wakandarasi wawili, mara ya kwanza ujenzi ulifanywa na Mkandarasi M/S Lukolo Company LTD aliyeingia mkataba na Halmashauri wa kujenga KM 8.6 za barabara kwa kiwango cha lami nzito kwa gharama ya Tshs 14, 320,586,464.39 ikijumlishwa na VAT. Gharama hiyo ya mkataba ilifanyiwa mapitio(revised contract ) na kufikia Tshs 11,933,899,897.09 ikijumlishwa na VAT. Muda wa Mkataba ulikuwa ni miezi 24, ambapo mkataba ulivunjwa tarehe 09/10/2017 baada ya Mkandarasi kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati kulingana na mkataba.
Ujenzi wa barabara mara ya pili, ulianza tarehe 25/03/2018 baada ya kazi kutangazwa upya na kumpata mkandarasi CHINA SICHUAN INTERNATIONAL CORPORATION (SIETCO) ambaye anatekeleza mradi kwa kasi inayokubalika na sasa unatarajiwa kukamilika tarehe 30/09/2019.
Mradi huu mpaka kukamilika utagharimu jumla ya Tshs 13,164,965,966 Mpaka sasa kiasi cha fedha kilicholipwa ni Tshs 6,038,006,039.65na gharama ya Mhandisi mshauri ni Tshs 337,000,000 kati ya fedha hizo amelipwa 159,500,000.00.
Mpaka sasa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 85 ya utekelezaji ambapo, barabara ya FFU – Matogoro yenye urefu wa 3.2KM imewekwa Lami nzito (Asphalt Concrete) na barabara zilizobaki zipo kwenye hatua ya kuweka tabaka la kokoto(CRR). Mifereji imejengwa katika baadhi ya barabara na kazi ya kujenga inaendelea.
Mradi mwingine ni Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Ruvuma.Ujenzi wa kituo cha Afya Ruvuma ulianza 24/07/2018 na unafanyika kupitia mafundi wadogo. Mradi wa huu hadi kukamilika utaghalimu shilingi 400,000,000 mapaka sasa mradi umefikia asilimia 99.M majengo yote manne ambayo ni Wodi ya akina mama, Maabara, jengo la mapokezi na jengo la upasuaji yamekamilika kazi za ukamilishaji milango zinaendelea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa