MJI wa Songea uliopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,ulianzishwa mwaka 1897 kama Kituo cha Kijeshi cha Kijerumani,mji huo ulikuwa Makao makuu ya utawala wa wakoloni wa kijerumani na wilaya ya Songea.
Tangu wakati wa utawala wa kikoloni hadi sasa Mji wa Songea umeendelea kuwa makao makuu ya mkoa wa Ruvuma.Mji wa Songea una umaarufu wa mashujaaa waliopigana vita vya Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 ambapo mashujaa 67 walinyongwa mwaka 1906 na kuzikwa katika kaburi moja ambapo Nduna Songea Mbano(Picha ya kwanza kushoto iliyopigwa na wajerumani mwaka 1906 muda mchache kabla ya kunyongwa).
Songea Mbano ambaye mji wa Songea umepewa jina lake, kutokana na umaarufu wake ,alinyongwa na kuzikwa katika kaburi la pekee yake eneo la Mashujaa wa Majimaji Mahenge mjini Songea.
Mji wa Songea ulizinduliwa rasmi kuwa mji wa kihistoria,kishujaa na kiutalii mwaka 2010.Mji huo ni miongoni mwa miji michache nchini yenye hazina kubwa ya utajiri wa historia ya utajiri katika nchi yetu.Manispaa ya Songea inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 260,106 wakiwemo wanaume 124,340 na wanawake 137,171 kutokana na ongezeko la asilimia 4.4 kwa mwaka.
Manispaa ya Songea yenye mitaa 95 na kata 21 ina jumla ya kaya 61,930 kwa wastani wa watu 4.2 katika kila kaya.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa