Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
12 MACHI 2022.
“Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya masoko 11, kati ya masoko hayo ni masoko 7 ambayo yanatoa huduma ambapo miongoni mwa masoko hayo ni pamoja na soko la Manzese A na Manzese B ambayo yanatarajia kuboreshwa miundombinu yake kupitia mradi wa kuboresha miundombinu na utendaji kazi ndani ya Halmashauri za Miji (TACTIC)”.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko katika kikao kazi cha mapitio ya utekelezaji wa miradi ya TACTIC, kilichofanyika hapo jana tarehe 11 Machi 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake Mhandisi na Mtaalamu wa mipango miji kutoka Benki ya dunia nchini, Eng. Fredrick Manase Nkya alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huo kati ya Halmashauri za miji 12 katika kipindi cha awamu ya kwanza.
Sambamba na utekelezaji miradi hiyo kutakuwa na uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami (Km 9.5) pamoja na maeneo ya kutupa taka, ambapo utekelezaji wa miradi hiyo unatarajia kuanza hivi karibuni. “Nkya alieleza”
Jumla ya shilingi Trilioni moja na Bilioni 150 zimetolewa kutoka Benki kuu ya dunia ambazo zitagawanywa katika Halmashauri za Miji 45, kwa lengo la kuboresha miundombinu mbalimbali ili kupunguza changamoto ya upungufu wa miundombinu bora katika Miji ya Tanzania.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa