MRADI huu uliopo katika kata ya Tanga Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, ulianza kutekelezwa Julai, 2017,hadi sasa ujenzi wa machijio ya kisasa umekamilika kwa asilimia 100 ambapo makabidhiano ya mradi yamefanyika Juni 13 kwa Mkandarasi kukabidhi mradi katika Kamati ya Fedha na Uongozi. Gharama ya mradi huu ni jumla ya shilingi. 3, 216, 237,382.4 ambapo Mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa zaidi ya bilioni 1, 924, 419,648.4 Machinjio hii itakapokamilika itaongeza idadi ya ng’ombe wanaochinjwa katika Manispaa kutoka Ng’ombe 32 kwa siku mpaka Ng’ombe 200 kwa siku na kuongeza ubora wa bidhaa za nyama.
Machinjio hii inatajwa kuwa ndiyo machinjio inayoongoza kwa ubora zaidi katika Tanzania ambayo inatarajia kufungua fursa za ajira na kuongeza uchumi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa