Na. AMINA PILLY
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
‘’Wananchi hawana taarifa sahihi kuhusu chanjo ndio maana mwamko wa wananchi katika swala la kuchanja ni dogo hivyo tunatakiwa kuimarisha dhana ya mawasiliano na kuwafanya wananchi wengi waweze kupata tarifa sahihi na kubadilisha fikra potofu walizonazo na wakubali kuchanja”
Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga wakati akifungua mafunzo kwa timu ya wataalamu wa afya Mkoani Ruvuma inayohusu utoaji wa huduma za chanjo kwa wananchi kwa lengo la kufanya uhamasishaji wa chanjo na kutoa elimu kwa wananc
DKT. Khanga amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wasikivu wakati wa mafunzo yayonaendelea kutolewa katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kuanzia jana 24-25/9/2021 kwa wataalamu wa afya kutoka katika Halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwajengea uwezo namna ya kuhamasisha jamii na utoaji wa huduma ya chanjo.
Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipokea chanjo 1,058,400 kitaifa, ambapo zoezi hilo la utaji chanjo lilizinduliwa kitaifa tarehe 07 julai Jumla ya wananchi 27 mwezi julai 2021, ambapo Mkoa wa Ruvuma ulipokea chanjo 30,000 na hadi hivi sasa kwa kushirikiana na Boresha afya wameweza kufanikiwa kuchanja chanjo 7826.
Aliongeza Mkoa wa Ruvuma ulianza kutoa chanjo tarehe 03 agost 2021 huku kukiwa na vituo maalumu vya kutolea huduma za chanjo 23 lakini kupitia huduma Mpango Shirikishi na Harakishi umekwenda kuboresha Zaidi na kuhamasisha jamii kupata chanjo ambapo kwa sasa Mkoa wa Ruvuma umeongeza vituo 200 kwa kutoa huduma ya chanjo.
Naye kiongozi wa timu ya kitaifa ya chanjo katika mkoa wa Ruvuma William Reuben amewataka washiriki wa mafunzo kuleta matokeo chanya katika kazi watakazotakiwa kwenda kuzifanya ili kutekeleza lengo la saerikali la kuhakikisha wananchi wake wanapata chanjo .
Mpango shirikishi na Harakishi
JIKINGE, IKINGE NA JAMII INAYOKUZUNGUKA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa