MKOA wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano nchini inayoongoza kwa udumavu na utapimlo hapa nchini.
Takwimu zinaonesha kuwa udumavu kitaifa ni asilimia 34 ambapo katika mkoa wa Ruvuma udumavu umefikia asilimia 44.4,licha ya kwamba mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.
Takwimu zinaonesha kuwa mkoa wa Ruvuma pia unakabiliwa na utapiamlo.Hali hiyo ndiyo iliyosababisha wadau wa lishe kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau wa lishe toka Halmashauri za Manispaa ya Songea,Halmashauri ya wilaya ya Songea na Ofisi ya Mkuu wa mkoa kukutana kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea katika mafunzo maalum ya lishe.
Mada za mafunzo hayo ziliendeshwa na wawakilishi kutoka TAMISEMI ambao ni Alan Bendera na Anna Andrew Afisa Liche kutoka TAMISEMI.
Alan Bendara Mtaalam wa Uchumi kutoka TAMISEMI ameagiza wazazi na walezi kuwekeza kwa siku 1000 za ukuaji wa motto ili kuepukana na udumavu na utapiamlo na kwamba elimu sahihi ya kukabiliana na tatizo hilo inatakiwa kutolewa katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Rajabu,Mtiula amesema wenyeviti wa Halmashauri walikuwa hawana uelewa kuhusu lishe na kwamba baada ya kupata mafunzo hayo sasa watahakikisha bajeti ya 2019/2020 inaongezeka.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Godfrey Chipakapaka amesema kuanzia sasa atahakikisha kuwa bajeti ya lishe inakuwa kubwa ili kukabiliana na udumavu na utapiamlo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema ameagiza hatua zichukuliwe ili kukabiliana na udumavu kwa sababu mkoa wa Ruvuma miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa udumavu.
Amesema Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ,amesaini mkataba wa lishe dhidi ya wakuu wa wilaya na kwamba wakuu wa wilaya nao wamesaini mikataba ya lishe na wakurugenzi wa Halmashauri.
Ameagiza elimu ya lishe itolewa katika makundi yote ili kukabiliana na vita ya udumavu.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Novemba 16,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa