MKOA wa Ruvuma umezalisha tani 1,255,134 na kuufanya Mkoa wa Ruvuma kushika nafasi ya kwanza Tanzania kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo baada ya kuzalisha kwa zaidi ya asilimia 200.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza wakati anafungua mkutano wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Ruvuma RCC amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Mkoa wa Ruvuma umenunua mazao ya ufuta,mbaazi na soya kupitia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani na kusaidia kupatikana kwa zaidi ya shilingi bilioni 27.87 ambapo mapato ya ufuta ni zaidi ya shilingi bilioni 25,soya zaidi ya bilioni 2.2 na mbaazi ni shilimgi milioni 542.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma umeendelea kushirikiana na Taasisi nyingine kusimamia zoezi la ununuzi wa korosho kutoka kwa wakulima ambapo hadi sasa jumla ya minada mitatu ya korosho imefanyika na kufanikiwa kuuza kg 6,894,985 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 18 na kwamba matarajio ya mavuno ya korosho kwa mwaka huu ni kilo 20,000.
Amesema mafanikio ya ulalishaji katika kilimo yanatokana na matumizi bora ya pembejeo za kilimo na kwamba katika msimu wa mwaka 2019/2020 serikali itaendelea na mfumo wa bei elekezi ya kun unua pembejeo za kilimo hususan mbolea ya kupandia na ya kukuzia ambapo Wizara ya kilimo na Mamlaka ya udhibiti wa ubora wa mbolea Tanzania imetoa bei elekezi kwa kila wilaya katika Mkoa wa Ruvuma.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa