MKURUGENZI mtendaji wa wilaya ya Nyasa Jimson Mhagama amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kujenga miundombinu ya miradi ya maendeleo kwa kuchangia nguvu zao kuanzia msingi hadi lenta ili kuunga juhudi za Serikali badala ya kuiachia serikali peke yake.
Aliyasema hayo hivi karibuni akiwa katika kata ya lipingo Wilayani hapa akiwa katika ziara ya kujitambulisha kwa watumishi na wananchi na kukagua ujenzi wa zahanati ya Ngindo iliyopo katika kata hiyo.
Mhagama alifafanua kuwa wananchi wana kila sababu ya kuhakikisha kuwa wanajitoa kwa kuchangia miradi ya maendeleo ili kuwe na maendeleo, na wananchi wakichangia nguvu zao wanakuwa na uwezo wa kujenga miundombinu na kutatua kero zilizoko katika maeneo yao kwa kuwa inakuwa imeshirikisha jamii.
Aliongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuibua miradi ya maendeleo ambayo ni kero katika kata au kijiji na kuanza kujenga hadi kufikia lenta na hatimaye Serikali itaezeka na kununua vifaa vya viwandani na kukamilisha miundombinu hiyo.
Alitoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Ngindo kata ya Lipingo kujitoa na kuendeleza ujenzi wa Zahanati ambayo imefikia ngazi ya msingi ili wajenge hadi ngazi ya lenta ndipo Serikali itaweza kukamilisha jengo hilo.
“wanajamii wa kata ya Lipingo tunatakiwa kujitoa kwa kuchangia ujenzi huu wa Zahanati ya Ngindo ambao upo ngazi ya msingi serkali haiwezi kukamilisha kwa hapo mlipofikia,mnatakiwa kuongeza juhudi za hali na mali kwa kuwa serikali iko nyuma yenu. Na mkichangia ujenzi huu hata jamii inakuwa na ari ya kutunza miundombinu hii hata mtu akitaka kuiba dirisha wote mtamzuia lakini ikijenga serikali peke yake hamtakuwa na uchungu wa aina yoyote”.alisema mkurugenzi huyo.
Alitoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Ngindo kata ya Lipingo kujitoa na kuendeleza ujenzi wa Zahanati ambayo imefikia ngazi ya msingi ili wajenge hadi ngazi ya lenta ndipo Serikali itaweza kukamilisha jengo hilo.
Awali Diwani wa Kata ya Lipingo Casbetth Ngwata kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo alimuomba Mkururugenzi Mhagama kutatua kero ya ujenzi wa Zahanati ya Lipingo kwa kuwa imekaa kwa muda mrefu bila kuendelezwa ikwa imefika hatua hiyo ya msingi na hamna juhudi zinazofanywa na wananchi katika kuliendeleza jengo hilo.
Wananchi hao waliahidi kujitolea nguvu zao na kuhakikisha jengo hilo linafikia hatua ya lenta ili Serikali iweze kukamilisha na kuanza kutumia Zahanati hiyo ikiwa inalengo la kutatua kero ya wananchi wa kata hiyo kwa kuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa