Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Wakili. Bashir Muhoja ameongoza kikao kazi cha Watumishi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazohusu watumishi nwa Halmashauri hiyo.
Hayo yamejiri tarehe 20 januari 2025 katika kikao kazi cha watumishi wa Halmashauri hiyo kilichofanyika kwa lengo la kupokea kero na changamoto zinazohusu watumishi wa Halmashauri ya hiyo ambacho kilifanyika katika ukumbi Shule ya Wasichana Songea
Wakili Muhoja alisema lengo la kikao hicho ni kuwataka watumishi wake waseme changamoto zinazowahusu mahala pa kazi ili aweze kuzifanyia ufumbuzi.
Miongoni mwa changamoto au kero zilizoibuliwa ni pamoja na Upungufu wa vitendea kazi (usafiri), Maslahi ya watumishi,maboresho ya miundombinu ya ofisi, haki na wajibu, nidhamu na mavazi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo, ambacho kitakuwa kinafanyika kwa kila robo ya mwaka
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa