Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amewataka watumishi kuendelea kufanya mazoezi mara kwa mara ili kulinda afya ya akili, na kimwili na kujenga mahusiano baina ya mtumishi na mwtumishi mwingine.
Amesema hayo siku ya tarehe 12 Januari 2024 ikiwa ni siku maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa Manispaa ya Songea iliadhimishwa kufanya mazoezi ya viungo ikiwemo na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu, mpira wa pete, mbio fupi pamoja na kuvutana kamaba sambamba na mapokezi ya watumishi wa ajira mpya, kuwaaga watumishi wastaafu na kuwakaribisha watumishi waliohamia kwa lengo la kudumisha upendo na mahusiano bora mahala pa kazi.
Sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa Bombambili.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa