MKURUGENZI wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI,Julias Nestory amewaagiza maafisa Elimu wa Halmashauri ya Songea Vijijini kufuatilia barua za upandishwaji madaraja kwa walimu kwa muda wa wiki mbili.
Ametoa agizo hilo wakati anazungumza na wadau wa elimu hao Katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Agosti15,2018.
Kikao kilichohudhuriwa na Maafisa Elimu,Wakaguzi wa shule kutoka Halmashauri zote na Walimu. Nestory ameapa kuchukua hatua endapo Afisa Elimu huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo.
Nestory pia amewashauri Maafisa Elimu Mkoa wa Ruvuma kufanyiwa uchunguzi kwa kina kabla ya kupewa nafasi za juu. Na pia asikitishwa na kitendo cha kuteua baadhi ya Wakuu wa shule kupata nafasi hizo kwa Rushwa za pesa, ngono na mambo mengine.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Ephrahim Simbeye akiongea mbele ya Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI ameahidi kutekeleza aagizo la Mkurugenzi kwa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Songea vijijini kwa kina.
Simbeye amesema anawatambua Wakuu hao wa shule waliopata nafasi hizo kwa njia ya Rushwa na hivyo bado anafanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa suala hilo.
Imetolewa na,
Victoria Ndejembi ,
Kitengo cha TEHAMA Manispaa Songea,
16 Agosti 2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa