MKUTANO WA UJIRANI MWEMA KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI ULIVYOIMARISHA USHIRIKIANO
MKUTANO wa ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika kwa siku mbili kuanzia Julai 23 hadi 24 mwaka huu kwenye hoteli ya Hunt Club Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma nchini Tanzania, umeimarisha mahusiano, undugu na kujenga ushirikiano baina ya nchi husika.
Katika mkutano huo maazimio 12 yanayozihusu nchi hizo yamepitishwa na yanahitaji utekelezaji ambao utaonesha matokeo makubwa katika maeneo ya Utawala bora, uchumi,biashara,ulinzi na usalama.
Maazimio ambayo yamepitishwa katika kikao hicho ni kuwaelimisha wananchi wanaovuka mipaka kutumia mipaka halali ili wananchi watumie mipaka na kuwezesha serikali zote kupata kodi,kuajiri wafanyakazi wenye weledi na masuala ya forodha na wafanyabiashara toka pande zote mbili kuanzisha maonyesho ya biashara ya ndani na nje ya nchi husika.
Maazimio mengine yaliopitishwa ni kutambua vituo vya mipakani viwe rasmi,kuwe na kituo cha pamoja ili kuboresha mazingira bora ya biashara,kuimarisha na kulinda mazingira kupitia mradi wa bonde la ziwa Nyasa na kutambua mapito muhimu ya wanyamapori ili kuzuia ujangili.
Kikao hicho pia kimepitisha maazimio ya kuzuia wizi wa pikipiki kupitia mipakani baina ya nchi hizo,wizi wa uuzaji wa silaha toka nchi zote,ununuzi wa boti katika mpaka wa Kilambonamoto ambao ulikuwa unafanyakazi upande wa Tanzania ili boti hiyo ianze kazi upande wa Msumbiji.
Maazimio mengine yaliopitishwa katika kikao hicho ni vikosi kazi vya usalama katika nchi husika kushirikiana kuchunguza wageni wanaoingia katika nchi hizo ili kuzuia viashiria vya uwepo wa matukio ya ugaidi.
Pia mkutano huo wa siku siku mbili umepitisha uwepo wa uvunaji haramu wa maliasili za madini ili ufanyike ufuatiliaji wa mara kwa mara kuwafuatilia wahusika wakamatwe na kuhukumiwa kulingana na sheria za nchi husika.
Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa wilaya na mikoa ya Ruvuma na Mtwara kwa upande wa Tanzania na wakuu wa wilaya na magavana wa majimbo ya Niassa na CaboDelgado kwa upande wa Msumbiji.
Kikao hicho muhimu pia kimehudhuriwa na mabalozi wa Tanzania nchini Msumbiji na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania.
Hiki ni kikao cha tatu cha ujirani mwema kufanyika baina ya nchi husika. Mkutano wa kwanza ulifanyika mkoani Mtwara nchini Tanzania, Mkutano wa pili ulifanyika Pemba jimbo la CaboDelgado nchi Msumbiji ambapo mkutano wa nne unatarajiwa kufanywa Novemba mwaka huu katika Jimbo la Niassa nchini Msumbiji.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa