Ktibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Komredi James Mgego amewataka wananchi, wanachama wa CCM Mkoani Ruvuma pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali kushiriki Mkutano mkubwa uatakaofanyika tarehe 08 februari 2025 katika uwanja wa shule ya Msingi Mtarawe ambao ni utekelezaji wa azimio la Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao uliazimia kumteua Dkt Samia Suluhu Hassan na Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa uchaguzi 2025.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 06 februari 2025 katika ofisi ya chama cha mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini, ambapo shughuli hiyo itafanyika kwa kushirikiana na majimbo matatu ikiwemo Jimbo la Peramiho, Mdaba na Songea mjini ambapo itaanza na maandamano ambayo yatagawika katika makundi manne.
Maandamano yataanza saa 2;00 kamili asubuhi kuelekea kwenye uwanja wa Shule ya Matarawe.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa