Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Labani Thomas amewataka Wakuu wa Wilaya Mkoani Ruvuma kufanya ziara ya kuwatembelea Wananchi kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitatua pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
kauli hiyo imetolewa leo tarehe 31 Januari katika Tafrija ya Kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Wilmani Kapenjama Ndile iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma iliyohudhuriwa na viongozi ngazi ya Mkoa, Halmashauri, pamoja na wataalamu mbalimbali.
Kanal Laban alisema “ tekelezeni maagizo yaliyotolewa na Chama cha Mapinduzi ambayo yanawataka Wakuu wa Wilaya kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo na kutatua migogoro na malalamiko ya wananchi.
Aliongeza kuwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma sio wavivu ni wakulima hivyo amewataka kusimamia changamoto zote zinazowakabili wakulima na kuzipatia ufumbuzi na endapo mtashindwa kutekeleza maagizo hayo mtakwamisha maendeleo. “Kanal. Laban aliagiza. “
Ametoa Rai kwa wataalamu Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanasimamia zoezi la wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti ambapo ni asilimia 63% ya wanafunzi wameripoti shuleni.
Naye mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amewataka Wakuu wa Wilaya wapya kutoa ushirikiano katika kusimamia shughuli za maendeleo katika Halmsahauri ili kutekeleza lengo la Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 sambamba na utunzaji mazingira.
Akizungumzia sakata la migogoro ya wafugaji ambayo ni kero kwa jamii ambapo alisema nanukuu” Mkoa wa Ruvuma umejikita na kilimo sio Mifugo jambo ambalo amewataka Vongozi hao kutatua changamoto hizo iwezekanavyo.
Naye aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema alitoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Meya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi pamoja na wataalamu mbalimbali katika kipindi chake cha uongozi alishirikiana nao na kufanikiwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo, “ Pololet Alishukuru”
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea (Mteule) Mheshimiwa Wilman Kapenjama Ndile ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea ambapo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na yuko tayari kujifunza wakati wote na kisha alimtakia safari njema Mkuu wa Wilaya ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa