Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaagiza wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma na wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia na kuhakikisha kuwa tovuti za Halmashauri na tovuti ya Mkoa wa Ruvuma zinatangaza mara kwa mara vivutio vya utalii na uwekezaji ili vifahamike ndani na nje ya nchi hivyo kukaribisha wawekezaji ambao watafika na kjuwekeza hivyo kufungua fursa nyingine katika Mkoa wa Ruvuma ikiwemo ajira kwa vijana.Mndeme ametoa agizo hilo wakati anazungumza katika tamasha la utalii wa fukwe la Mkoa wa Ruvuma ambalo limefanyoika Mjini Mbambabay wilayani Nyasa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa