Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi christine Mdeme akikagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba-bay kilometa 66 unaoendelea katika eneo la uwanja wa ndege Mbamba-bay,Wilayani Nyasa alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani Nyasa,hivi karibuni. (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Dkt Oscar Mbyuzi na kulia ni Ofisa mipango Wilaya ya Nyasa Jabir Chilumba.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi.Christine Mdeme amewataka wananchi kupambana na uvuvi haramu katika ziwa nyasa na kuwachukulia hatua watu wote wanatakaobainika kutumia kukiuka sharia ya kuvua samaki wadogo wadogo.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifanya mkutano wa hadhara katika Kituo cha afya Kihagara kata ya Kihagara mkutano uliokuwa ni wa kuongea na kutatua matatizo ya wananchi wa kata ya Kihagara ambao walipata fursa ya kutoa Kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata ya Kihagara.
Bi.Mdeme alifafanua kuwa tuna kila sababu ya kutunza maliasili zetu ili ziweze kuzifaidisha vizazi vyote vya sasa na vya baadae kwa kuwa kufanya hivyo kutatupelekea taifa letu kuwa na maendeleo hivyo aliagiza kuanzia sasa uongozi wa kijiji kulinda na kuhifadhi raslimali za uvuvi kwa kuhakikisha nyavu zote haramu zinakamatwa.
Mdeme aliwaonya wale wote wenye tabia ya kuvuna samaki wachanga kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa ni wauaji wa viumbe hai vinavyostahili kuishi kwa mujibu wa sharia na wananchi wote tunawafahamu wale wote wenye nyavu haramu kwa hiyo tunatakiwa kuwa waangalifu na hawa watu ambao wanaua samaki wetu.
“Naagiza kuanzia leo uvuvi haramu ni marufuku,uongozi wa Halmashauri, kata na vijiji naagiza tena marufuku mtu kuvua akiwa na nyavu haramu na kama akitokea nitakamata uongozi wote wa kijiji na kata na kuweka ndani kwa kuwa siamini uhalifu ufanyike ndani ya kijiji au kata viongozi wasiwe na taarifa ninachokijua watakuwa na maslahi na uvuvi haramu huo.
Wananchi wa kata hiyo ya kihagara walikubaliana na mkuu huyo na kumuahidi yote aliyose watayazingatia kwa kuacha na kutoa taarifa za walea wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alifanya ziara ya siku mbili hivi karibuni kwa kutembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo na kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kihagara Wilayani hapa.
IMETOLEWA NA
NETHO C.SICHALI
AFISA HABARI
NYASA DC
0783662568
|
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa