• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma azuia likizo kwa watendaji wakuu wa Mkoa na Wilaya

Tarehe ya kuwekwa: November 27th, 2018

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kuhakikisha mkoa wake unawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 wanapata nafasi ya kusoma kwenye madarasa ya kutosha,amesitisha likizo zote za watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari.

Mndeme ametoa agizo hilo jana wakati wa kikao chake na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vyumba vipya 142 vikamilike kujengwa

 Viongozi walizuiwa likizo  ni Katibu Tawala Mkoa,Wakuu wote wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri ,Afisa Elimu Mkoa na wale wa wilaya zote pia wahandisi wa ujenzi wa halmashauri.

“Nataka katika halmashauri zote zenye upungufu wa vyumba madarasa hakuna kiongozi kwenda likizo ya mwisho wa mwaka hadi madarasa mapya yakamilike kujengwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 waingie darasani ” alisema Mndeme

Awali akitoa taarifa fupi ya hali ya hali ya miundombinu ya madarasa Katibu Tawala Mkoa Prof Riziki Shemdoe alisema jumla ya wanafunzi wapya 1,556 watahitaji madarasa mapya ya kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari .

Prof.Shemdoe amezitaja halmashauri zenye upungufu wa madarasa na idadi kwenye mabano kuwa Tunduru(35),Mbinga  (18),Songea (09),Songea Manispaa (09),Namtumbo (26)

Halmashauri zingine zenye upungufu ni Nyasa  (32),Mbinga Mji (09) na Madaba (04)

Aidha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mndeme amezuia safari za mafunzo za madiwani wote katika halmashauri nane za Ruvuma hadi watoto wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hapo mwakani watakapoingia darasani..

Mwisho

Imetolewa na Afisa Habari

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma

Songea

27 .11.2018

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa