Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka wataamu wa Manispaa ya Songea kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya standi ndogo ya Ruhuwiko ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara y a kushitukiza katika kata hiyo ambapo alibaini kuwepo kwa baadhi ya changamoto kwenye stebdi hiyo ambazo zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka zaidi ikiwemo na ukarabati wa choo cha kulipia ambacho kinasimamiwa na Halmaashauri, kutjengwa kwa kibanda ndani ya stendi kwa ajili ya kukaa abiria wakati wanaposubili usafiri, pamoja na ukosefu wa maji safi katika maeneo hayo.
Ziara hiyo ya kushitukiza imefanyika tarehe 12 januari 2025 ambapo aliongozana na wataalamu wa Manispaa ya Songea kwa blengo la kufanya ukaguzi wa mazingira katika stendi hiyo huku akitoa muda wa wiki moja kuhakikisha wanatatua kero zote zilizopo kwatika Stendi ya Ruhuwiko
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa