MKUU wa wilaya ya Songea Pololet Mgema leo ameungana na wananchi wa Mtaa wa Mbarika Kata ya Mfaranyaki Manispaa ya Songea kushiriki katika usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi Oktoba.Pamoja na mambo mengine Mkuu wa wilaya amemuagiza Kamanda wa polisi wilaya ya Songea kumkamata mtuhumiwa anayedaiwa kula shilingi 800,000 ambazo zilichangwa na wananchi wa Mfaranyaki kwa ajili ya usafi wa Mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya usafi na Mazingira katika Manispaa hiyo Philipo Beno amesema mtuhumiwa huyo awali ilibainika kuwa alitumia zaidi ya shilingi milioni mbili ambazo zilichangwa na wananchi kwa shughuli zake binafsi kwa kuwa yeye amekabidhiwa mashine ya kukusanyia kiasi cha shilingi 2000 kwa kila kaya katika Mtaa wa Mbarika kata ya Mfaranyaki na kwamba alipobanwa amerejesha Manispaa shilingi milioni 1.2 na bado anadaiwa shilingi 800,000/=.
Kufuatia hali hiyo ndipo Mkuu wa Wilaya alimuamuru mtuhumiwa ambaye alikuwepo kwenye eneo la mkutano kukamatwa na kupelekwa katika vyombo vya Dola hadi atakapolipa kiasi hicho cha fedha anachodaiwa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa