Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile tarehe 23 Aprili 2024 amefanya ziara ya kutembelea shule za sekondari zenye wanafunzi wa kidato cha sita kwa lengo la kuwatia moyo wakielekea katika mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika May 2024.
Ziara hiyo imefanikiwa kwa kutembelea shule ya Sekondari Msamala, Shule ya Sekondari Dkt. Emmanuel Nchimbi, pamoja na shule ya Sekondari Londoni.
Akizungumza na wanafunzi wa Sekondari kwa wakati tofauti kiongozi huyo alisema “ Mtihani hujaza hofu kwa watainiwa kutokana na kusoma kwa miaka mingi lakini kwenye mtihani unaulizwa vitu vichache hivyo amewataka wanafunzi hao kujiamini na kumtanguliza mungu pamoja na kuzingatia masomo waliyofundishwa darasani na hatimaye watafaulu daraja la kwanza .” alibainisha.
Ndile aliongeza kuwa mkifanya vizuri katika mitihani yenu mtaleta sifa nzuri katika shule, na jamii mnayotoka, pia alitoa wito kuzingatia kanuni za usimizi wa mitihani ambapo amewataka kutogushi au kufanya udanganyifu katika mitihani ambayo kwa kufanya hivyo wanaweza kusababisha matatizo katika shule au watahiniwa wote.
Aidha, katika kuwatia moyo wanafunzi hao mkuu wa Wilaya ametoa kilo sitini 60 za mchele kwa kila shule aliyotembelea za kidato cha sita.
Kwa upande wa wanafunzi wametoa shukrani kwa Serikali kwa kuwajengea miundombinu bora, pia wameahidi kufanya vizuri katika mitihani yao.
Mwisho.
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa