NA;
AMINA PILLY
AFISA HABARI
MANISPAA YA SONGEA.
07.08.2022
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amewataka wananchi kufanya mazoezi kila siku kwa lengo la kulinda afya za mwili.
Akizungumza na wananchi katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea ambapo alisema lengo kuu la kufanya mazoezi ni kulinda afya ya mwili ikiwa mazoezi ni tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu.
Hayo yamebainishwa jana tarehe 06.08.2022 katika ofisi ya mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na wananchi, watumishi kwa lengo la kuhamasisha chanjo ya UVIKO 19 na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kupambana na UVIKO 19.
Aliongeza kuwa tarehe 23.08.2022 ni siku ya SENSA ya watu na Makazi hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani watakaokuwa wanapita kwenye kaya mbalimbali ili kuwezesha Serikali kupata takwimu sahihi za wananchi.
Naye Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dkt. Luis Chomboko alieleza kuwa lengo kuu la kufanya mazoezi ni kujenga afya ya mwili na kuhamasisha jamii ijitokeze kuchanja chanjo ya UVIKO 19 ambapo zoezi hilo linaendelea kufanyika katika uwanja wa Maji maji ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa kampeni ya Mziki Mnene ambapo hadi hivi sasa Mkoa wa Ruvuma umechanja chanjo ya UVIKO 19 zaidi ya 70%.
MWISHO
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa