Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile, amewataka watanzania kuendelea kuenzi muungano wetu na kudumisha amani huku akisisitiza kuwa matokeo ya jitihada za waasisi wa Taifa la Tanzania hazipaswi kupuuzwa.
Hayo yamejiri wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 61 ya muungano katika Wialaya ya Songea yaliyofanyika katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea ambapo yamehudhuriwa na wananchi mbalimbali, wazee, jeshi la polisi na wadau wa Mbalimbali kwa lengo la kudumisha na kuenzi muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo yalianza kwa kufanya usafi, kupanda miti pamoja na matembezi ya amani.
Ndile alisema, nchi nyingi duniani zimesamabaratika kutokana na kukosekana kwa mshikamano, huku akiwataka watanzania kuendelea kuwa na umoja na kulinda muungano na hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa wamoja licha ya tofauti zao, ambapo alieleza kuwa jukumu la kulinda muungano ni lakila mmoja. "Alibainisha."
Alihimiza umuhimu wa mazoezi ya mwili kama sehemu ya kujenga afya kwa watanzania nakuwa na jamii imara pia akisisitiza wananchi kuanza kufanya mazoezi ya kila wiki ili kupunguza gharama za tiba na kujenga ustawi wa maisha ya jamii.
Aliongeza kuwa viongozi wa taasisi zote kuendeleza mshikamano na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ili kuimarisha amani,na mshikamano kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mwisho.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly
Kitengo cha mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa