Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka Walimu wa kuu na Maafisa watendaji kusimamia miradi ya BOOST na kuhakikisha inakamilika ifikapo juni 30 2023 ambayo inajengwa katika shule saba 7 za Msingi kwa lengo la kuboresha miundo mbinu ya kusomea na kujifunzia ya Elimu Msingi na awali.
Hayo yamejili katika ziara ya Mkuu wa Wilaya iliyofanyika kwa siku moja kwa lengo la kukagua hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya BOOST ambayo inatekelezwa katika shule ya msingi Kipera, Shule ya Msingi Mbulani, Shule ya Msingi Ruhuwiko, Shule ya Msingi Matogoro, Shule ya Msingi Mkuzo, Shule ya Msingi Amani, Shule ya Msingi Bombambili.
Mhe. Ndile alisema Manispaa ya Songea imepokea Mil. 893 kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ikiwemo na ujenzi wa shule mpya hivyo amewataka wataalamu hao kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa