Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka Maafisa Watendaji Kata, Mitaa, Waratibu Elimu Kata, na Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kutoa ushiririkiano wa kutosha katika kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza, awali na darasa la kwanza wanaripoti shule.
Agizo hilo limetolewa tarehe 16 Januari 2024 katika kiako kazi cha kuhakiki takwimu za wanafunzi walioripoti shule kuanzia awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa wanafunzi hao.
Ndile amewataka maafisa watendaji kuhakikisha kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2024 awe ameripoti shule na mzazi yeyote atakayeshindwa kupeleka mtoto wake shule achukuliwe hatua za kisheria.
Amewataka wakuu wa shule, maafisa watendaji wa kata na Mitaa kufanya usafi katika ofisi zao na kuhakikisha wanasimamia usafi wa mazingira kwenye kaya pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kiako hicho kimepangwa kufanyika tena tarehe 02 Februari mwaka huu pia ameagiza kila mkuu wa shule alete takwimu sahihi za mahudhuriao ya wanafunzi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa