MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amewaongoza wakazi wa Kata ya Matarawe Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kufanya usafi wa Mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Julai 2019.Wengine walioshiriki katika usafi huo ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo na Diwani wa Viti Maalum Kata ya Matarawe Judith Mbongoro.
KATIKA utekelezaji wa agizo la Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli,linalosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea anawatangazia wananchi wote kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kushiriki katika usafi wa mazingira kwenye makazi,Taasisi,biashara,jumuiya na maeneo yote ya makazi kwenye mitaa na kata.Kwa wale wote ambao watabainika maeneo yao ni machafu watatozwa faini ya shilingi 50,000 au kufikishwa mahakamani.Kumbuka usafi ni tabia kila mmoja ajitokeze kwa hiari bila kulazimishwa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa